У вашего броузера проблема в совместимости с HTML5
Changamoto ya unywaji pombe imebakia kuwa kizingiti kikubwa kwa maendeleo katika baadhi ya maeneo humu nchini . Katika ripoti iliotolewa na shirika la takwimu nchini, kaunti ya Murang'a imeorodheshwa kuwa mojawapo ya maeneo ambayo yameathiriwa pakubwa na tatizo la unywaji pombe hasa kwa vijana. Ripoti hiyo pia inapendekeza kwamba iwapo kaunti hiyo inanuia kupambana na umaskini, basi ni lazima isuluhishe suala la unywaji pombe.