Mbunge wa zamani Mzindakaya azungumza baada ya kuzushiwa kufariki leo
У вашего броузера проблема в совместимости с HTML5
Asubuhi mapema ya leo April 13, 2017 kulizuka taarifa ambazo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kifo cha Mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa zamani wa Kwela 'CCM', Dkt. Crisant Mzindakaya.
Taarifa hizo zilieleza kuwa Dkt. Mzindakaya alifariki akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dkt. Crisant Majiyatanga Mzindakaya, aliingia Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1965 kama Mbunge wa Jimbo la Ufipa Kusini, lakini mbio zake ziliingia doa mwaka 1981 baada ya Mahakama kumvua Ubunge kutokana na ushindi wake wa mwaka 1980 alitumia faulu.