У вашего броузера проблема в совместимости с HTML5
Muhadharah wa Dini: SIRI ZA MAJINI NA WAGANGA ZAFICHULIWA. katika Qur'an na Sunna. Video hii ni katika mlolongo wa mihadhara iliyoandaliwa na Alnoor Islamic Centre - London kuhusu mada ya Majini na Waganga. Maalim Ahmad Mohamed Kassa, baada ya utafiti mrefu, anafichuwa siri ya viumbe hawa majini na uadui wao kwa wanadamu, uhusiano wao na waganga, Shirki inayofanywa na watu wengi kwa kuamini na kukubali majini, kutaka msaada, kinga na tiba kwa majini na kuwasiliana nao. Mafunzo yote haya ni kwa mujibu wa Qur'ani na Sunna. Yanayotakikana kwa Mwislamu ni kukataa uhusiano na majini, na kuacha kwenda kwa waganga NA KUMTEGEMEA ALLAH KATIKA KILA HALI YA MAISHA.